SULUHU YA KANSA YA TEZI DUME IMEPATIKANA SASA

TEZI DUME NI NINI?
Hii ni tezi (kokwa) ambayo inapatikana katika mfumo wa uzazi wa mwanaume katika shingo ya kibofu cha mkojo. Kazi yake kubwa ni kutengeneza maji maji ya uzazi kwa mwanaume(shahawa) ambayo husaidia kurutubisha mbegu za kiume zilizotengenezwa kutoka kwenye korodani na husaidia kusafirisha mbegu za kiume na kuzifanya zibaki hai kwa muda unaostahili.
Tezi hii huwa inaongezeka uzito au ukubwa kadri umri wako unavyozidi kukua. Na nimekwambia kuwa tezi hii ipo katika shingo ya kibofu cha mkojo na hivyo basi ukuaji wake unaweza kuathiri mfumo mzima wa utoaji mkojo kwenye kibofu(Incomplete bladder emptying) .
Tafiti zinaonesha kwamba tezi huanza kuongezeka uzito kuanzia miaka 25, na huendelea kukua kila siku kadri umri unavyo enda. Kuongezeka kwa uzito wa tezi yako ya kiume sio tatizo kimatibabu kwani kipimo cha kuonesha moja kwa moja umefikia hatua sio nzuri ni pale unapoanza kupata dalili zenye kuzuia mkojo kutotoka vizuri (obstructive symptoms). Hivyo uzuri ni kwamba kuanzia pale tezi inapokuwa inaongezeka ukubwa hadi kufikia kuonesha dalili mbaya ni hadi unapofikia angalau umri wa miaka 60 na kuendelea , pia inaweza hata ikatokea hata unapokuwa una umri chini ya miaka 50 inategemea na mwili wako kibaolojia. Basi kukua huku kwa tezi bila sababu ya msingi tunaweza tukawa na hitimisho la magonjwa makuu mawili au matatu,
Kwanza Benign Prostate Hypertrophy (BPH) aka Kukua kwa tezi dume,
 pili Prostate cancer Hii ni kansa ya tezi dume na 
Tatu Uvimbe kwenye kibofu cha mkojo.
Njia pekee ya kuyatenganisha magonjwa hayo matatu kwa wanaume ni kwa njia kuu mbili, Kwanza Chukua historia vizuri ya mgonjwa wako kuanzia alipo anza kuona dalili na angalia afya yake vzuri kabisa,Afya ni muhimu sana kwani moja ya dalili ya moja kwa moja ya kubaini kuwa mtu ana kansa ni kudhoofika kwa mwili wake, Hivyo historia ya mgonjwa ni muhimu sana. Mfano, Mgonjwa wa kuvimba kwa tezi dume atakuja ana umri wa miaka 69 analalamika mkojo unatoka kwa kudondoka kama matone matone hautoki katika mfululizo, pia anakwambia mkojo unakuwa unabaki kwenye kibofu na analalamika kiuno kinamuuma sana na UTI za mara kwa mara lakini ukimwangalia afya yake ipo vizuri hajadhoofika kwa lolote. Hivyo basi mgonjwa huyu moja kwa moja anakuwa ameangukia kwenye BPH na sio kansa ya tezi dume.
Mfano mwingine Anakuja mzee wa miaka 85 amedhoofika afya yake mbavu zote na mifupa ya usoni ipo nje, analalamika kuwa mkojo hautoki vizuri, anakojoa mara kwa mara na hamalizi mkojo wote kwenye kibofu na UTI za mara kwa mara, Hapo lazima akili yako impeleke mgonjwa wako kuwa ana Prostate Cancer.
Wagonjwa wengi pia wanaweza wakaja na dalili za uvimbe kwenye kibofu (bladder tumor) huwezi kubaini uvimbe kwenye kibofu kwa kupiga kipimo cha picha yoyote bali njia pekee ni kuchukua sampuli ya kipande cha uvimbe kwa kusaidiwa na kipimo kiitwacho Cystoscope (kipimo kinachopiga picha kibofu cha mkojo na kuona uvimbe live kwa kutumia screen iliyopo pembeni mwa mtaalamu wa vipimo. Moja ya dalili ambazo mgonjwa wa namna hii anaweza kukueleza ni kukojoa mara kwa mara ( Uvimbe kwenye kibofu unapunguza ukubwa wa kibofu hivyo kibofu kinajaa mara kwa mara) Pia wengi huja wakilalamika kuwa wanakuwa na historia ya kukojoa damu mwishoni anapokuwa anamalizia kusukuma mkojo. Na mara nyingi ukiwauliza makazi ya wagonjwa hawa utakuta wanatoka kando kando ya ziwa au ni wakulima sana wa mpunga au kilimo cha mbugani hii ni kwa sababu aina nyingi za kansa za kibofu cha mkojo hapa afrika husababishwa na wadudu aina ya Schistosoma Haematobium ambao husababisha KICHOCHO. Hivyo hakikisha unamuuliza mgonjwa wako kama ana hivyo vitu vihatarishi ingawaje vipo vingi hivyo ni baadhi.
 SWALI AMBALO WENGI HUJIULIZA
                               JE TEZI DUME NI SAWA NA MSHIPI WA NGIRI ?
Napenda kujibu kuwa hivyo ni vitu tofauti kabisa na matibabu yake tofauti kabisa. Kutokana na elimu ya tiba ya kizungu (convetional medicine) ugonjwa wa mshipa wa ngiri ni ugonjwa unahitaji operation kulingana na ngazi ugonjwa huo umefikia wapi ( Nitaeleza kidogo).
Hernia kwa lugha nyepesi ni ile hali ya viungo vya tumboni kujitokeza nje pamoja pamoja na ngozi na kutengeneza kama mfuko flani unaoning’inia. Kutokeza huku kunaweza kukawa kupitia kitovu ,pembeni ya kitovu au sehemu za siri (Inguinal hernia au ngiri). Hivyo kuna viungo ambavyo unaweza kujaribu kuvirudisha ndani vikakubali na baada ya muda, labda umekohoa vinatokeza tena (Reducible Hernia) na kuna hernia ambayo huwezi kuirudisha ikisha tokeza imetokeza ( Non reducible hernia). Nadhani umenipata kuwa ngiri ukitaka upate suluhisho la haraka onana na daktari wa upasuaji atakupa ushauri kama inahitaji upasuaji au laa! Sasa huwa nashangaa ninaona mtu anasema hernia inaweza kutibika bila upasuaji kwa kutumia dawa pekee, hivi unaweza kuniambia kuwa utumbo umetoka nje nikikupa dawa utumbo urudi ndani? Huo utakuwa ni upotoshaji na kutokubali kugawana majukumu kiutendaji.
Tezi dume sio ugonjwa , hio ni kokwa inayotenegeneza maji ya kiume (shahawa) Hivyo ukitaka umaanishe kuwa ni ugonjwa bora useme Ugonjwa wa tezi dume( Kukua/kansa), Hivyo nitafurahi wateja wangu mnaopenda kuniuliza maswali, unasema mimi nina dalili za tezi kukua, mimi nina dalili za kansa ya tezi dume. Hapo nitakuwa nimekuelewa na sio kusema mimi nina tezi dume, Wote wanaume tuna tezi dume.
 NINI  MAHUSIANO YA KUPATA KANSA YA TEZI DUME NA MATUMIZI YA MAZIWA NA BIDHAA ZITOKANAZO NA MAZIWA?
Tafiti zinaonesha kwamba kuna ongezeko kubwa sana la kupata kansa ya tezi dume pale unapofikia uzeeni. Mwaka 2011 tafiti zinaonesha kwamba ni Zaidi ya watu 200,000 walikuwa wamebainika kuwa na tatizo hili duniani. Kutokana na tafiti nyingi zimeonesha kuwa ongezeko kubwa la watu wenye kansa ya tezi ya kiume ni baada ya kuhusianisha ugonjwa wa kansa ya kiume ( prostate cancer) na matumizi ya maziwa na bidhaa zote za maziwa na pia nyama nyekundu zimeonesha uhusiano mkubwa sana katika kusababisha kansa ya tezi dume.
MAHUSIANO YENYEWE

SULUHU YA KANSA YA TEZI DUME IMEPATIKANA SASA SULUHU YA KANSA YA TEZI DUME IMEPATIKANA SASA Reviewed by Koroti MlMProTz on 9:13 PM Rating: 5

No comments: