TATIZO LA KUWASHWA SEHEMU ZA SIRI KWA WANAWAKE/VAGINAL ITCHING:
Kwa kawaida kuwashwa sehemu za siri husababishwa na maambukizi ya fangasi au maambukizi mengine ya bacteria katika sehemu husika.Wakati mwingine mzio(allergy) pia inaweza kusababisha muwasho katika sehemu za siri.
-Muwasho maeneo ya ndani ya uke au kwenye mashavu ya uke husababishwa na mambo mengi. Muwasho ndani ya uke (vagina) unaweza kutokana na;
1.Matumizi ya kemikali au sabuni zilizowekewa dawa ya kuua bakteria ( detergents or medicated soaps),
2.Kwa kuosha ndani ya uke kwa sabuni zenye dawa ya kuua wadudu au kuondoa harufu (kitaalamu tunasema vaginal douching) na kitendo hiki hupelekea kuua bakteria wanaoishi kwenye uke (normal flora) kwa ajili ya kuulinda,
3.Kwa kutumia cream au manukato kwenye uke,
4.Kwa kutumia sabuni za bafuni(bath products)kwa kunawia maeneo hayo nyeti.
5. Wanawake ambao wameacha kuingia kwenye hedhi wanaweza kupata mwasho kutokana na kubadilika kwa kiwango cha homoni ya Oestrogen. Kwa kipindi hiki kuta za uke huwa nyembamba na kukauka na hivyo kupelekea kupata miwasho.
NAMNA GANI TUNAWEZA KUZUIA MWASHO SEHEMU ZA SIRI?
Wanawake wanatakiwa kuchukua hatua zifuatazo kuzuia mwasho sehemu za siri:
1.Namna ya kujitawaza baada ya haja ndogo au kubwa: Wanawake wanashauriwa kujitawaza kutokea mbele kuelekea nyuma ili kuzuia bakteria wa kwenye njia ya haja kubwa(anus) kuingia kwenye uke (vagina)
2.Kuzuia matumizi ya kemikali au sabuni zilizowekewa dawa ya kuua bakteria (detergents or soaps), kuosha ndani ya uke kwa sabuni zenye dawa ya kuua wadudu au kuondoa harufu (kitaalamu vaginal douching), kutumia cream kwenye uke, karatasi za chooni (toilet papers) na sabuni za bafuni (bath products)
3.Kuhakikisha sehemu za siri ni kavu baada ya kujisaidia au kuoga.
4.Kutokuvaa nguo za ndani ambazo hazibani sana (Wear loose natural fiber underwear and clothing)
5.Hakikisha sehemu za siri ni safi na kavu wakati wote,
6.Zuia kukaa na nguo zenye unyevunyevu kwa muda mrefu, 7.Jiepushe kufanya ngono zembe.
8.Tumia pedi bora zilizotengenezwa kwa teknolojia ya hali ya juu(anion chip technology) ili kujikinga na kujiepusha na miwasho na michubuko sehemu za siri pamoja na UTI.(Machukizo mbalimbali wakati wa hedhi)
KWA MAHITAJI YA PEDI HIZI WASILIANA NASI: 0656459057-calls & whatsapp.
Koroti
Health Consultant
Karibu sana.
SULUHU YA KUWASHWA UKENI
Reviewed by Koroti MlMProTz
on
10:07 AM
Rating:
No comments: