KUNUKA MDOMO (Halitosis)
Urembo na Utanashati wako hautakua kamili kama unanuka mdomo. wengi husumbuliwa na tatizo la kunuka mdomo bila hata kujijua hivyo kuwa kero na hujishushia hadhi mbele ya jamii basi leo ndugu yangu nimekuletea somo hili ili uweze kuepukana na tatizo hili la kunuka mdomo
SABABU ZA KUNUKA MDOMO
• uchafu wa kinywa , kutozingatia kanuni za kusafisha kinywani
• Vyakula tunavyokula, baadhi ya vyakula mfano vitunguu huleta harufu mbaya kinywani
• Bidhaa za tumbaku(sigara nk)
• Kukauka kwa mate, kwenye mate kunakua na bakteria wazuri ambao hulinda kinywa, mate kukauka huwaua hawa bakteria wazuri na kufanya wabaya kutawala hivyo kuleta harufu mbaya
• Hali ya kiafya au maambukizi katika pua ,maskio, mdomo ,koo pamoja na tumbo, viungo hivi vinaingiliana hivyo uchafu katika pua ,maskio ,koromeo na tumbo huweza kuleta harufu mbaya kinywani ,pia maambukizi ya fangasi mdomoni ,kooni na tumboni pia matatizo mbalimbali ya tumbo mfani: kukosa choo nk huchochea harufu mbaya kinywani
• baadhi ya magonjwa mfano baadhi ya Vidonda ndugu (cancer)
MAMBO YA KYFANYA UKIWA NA TATIZO
• safisha kinywa kwa kupiga mswaki angalau asubuhi na usiku kwa kutumia dawa sahihi ya meno, pia sukutua kwa maji safi kila baada ya kula chochote hata ukinywa juice. Wakati wa kupiga mswaki hakikisha unaupitisha maeneo yote pia katika fizi na ulimi
•kunywa maji kwa wingi kwani husaidia kutatua matatizo mengi mfano kukauka kwa kinywa na kutopata choo.
•Pata matibabu kwa matatizo yanayokukabili katika mfumo mzima wa chakula na upumuaji
Kwa matibabu ya mfumo wa chakula kama choo kigumu,vidonda vya tumbo wasiliana nasi
Text/Whatsapp 0656459057
Koroti
Health Consultant
Pia subscribe kwenye blog yangu na uniadd rafiki
SABABU ZA KUNUKA MDOMO(HALITOSIS) NA SULUHU ZAKE
Reviewed by Koroti MlMProTz
on
8:19 PM
Rating:
No comments: